Latest Articles

RAIS DKT. MWINYI: TAMASHA LA KIZIMKAZI NI JUKWAA LA UTAMADUNI, UTALII NA FURSA ZA UWEKEZAJI

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Tamasha la Kizimkazi limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kutangaza utamaduni, utalii, biashara na fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar, sambamba na kuchochea maendeleo ya wananchi.


Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 12 Agosti 2026, alipokuwa akizindua rasmi Tamasha la Kizimkazi 2026 lenye kaulimbiu “KIZIMKAZI Kumenoga!” katika Mkoa wa Kusini Unguja.


Amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maono ya kuasisi Tamasha hilo, ambalo limekuwa likichangia kuhifadhi mila na utamaduni, kukuza utalii na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.


Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kutumia Tamasha hilo kutangaza fursa za uwekezaji katika utalii, uvuvi, mwani na Uchumi wa Buluu, huku Serikali ikiendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na miundombinu ya uzalishaji.


Amesema Tamasha la Kizimkazi linaunga mkono dhamira ya Serikali ya kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Zanzibar kutoka 800,000 hadi milioni 1.5, kupitia matukio maalum ya utalii na utangazaji wa vivutio, utamaduni, vyakula na ukarimu wa Wazanzibari.


Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza waandaaji, wadhamini, taasisi za Serikali, Sekta Binafsi, wajasiriamali, wasanii, wanamichezo na wananchi kwa kufanikisha Tamasha la Kizimkazi 2026, akihimiza kuendelea kulitumia kama jukwaa la kufungua fursa mpya za maendeleo.

Tamasha hilo linaendelea hadi tarehe 14 Agosti 2026, ambapo kilele chake kitafanyika katika Uwanja wa Mwehe, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.

















read more

MWENYEKITI WA CCM TAIFA NA RAIS DKT. SAMIA AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA WA MASKANI KATA YA KISONGE, MICHENZANI ZANZIBAR




Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanachama wa Chama hicho katika Maskani Kaka Kisonge, Michenzani Zanzibar, tarehe 11 Agosti, 2026.

Shamra shamra za Mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwasili Maskani Kaka Kisonge, Michenzani Zanzibar, tarehe 11 Agosti, 2026.




read more

JKCI YATAKIWA KUENDELEZA KAMBI ZA MATIBABU YA MOYO NCHINI COMORO

 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imetakiwa kuangalia namna ya kupeleka huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo nchini Comoro kutokana na huduma hizo kutopatikana nchini humo.


Rai hiyo imetolewa leo na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Dkt. Salim Hamad alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge kuona namna ambavyo huduma zinazotolewa na JKCI zinaweza kuwakomboa wananchi wa Comoro.


Dkt. Hamad alisema baada ya JKCI kuweka kambi maalumu ya matibabu ya moyo katika kisiwa cha Anjouan kilichopo nchini Comoro uongozi wa kisiwa hicho umeitaka JKCI kuingia mkataba nao wa kuendelea kufanya kambi za matibabu jambo ambalo linaonesha umahiri wa huduma zinazotolewa na wataalamu wa JKCI.


“Nilifurahi nilipokutana na uongozi wa kisiwa cha Anjouan na kuniomba niwajulishe kuwa wanataka tuingie nao mkataba wa kufanya kambi za matibabu, hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu katika kutoa huduma bingwa za matibabu ya moyo”, alisema Dkt. Hamad.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema uhitaji wa huduma za matibabu ya moyo nchini Comoro ni mkubwa kutokana na mwitikio uliokuwepo wakati wa kambi ya matibabu iliyofanyika mwezi Oktoba mwaka jana katika kisiwa cha Anjouan.


“Tunaandaa mkakati wa kuitangaza JKCI nchini Comoro ili tuweze kuwasaidia wananchi wa Comoro kufahamu zaidi huduma tunazozitoa na kuwapunguzia adha ya kuzifuata huduma hizi mbali na nchi ya Comoro”, alisema Dkt. Kisenge.



read more

IAEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUSAFIRISHA MABAKI YA VYANZO VYA MIONZI ORCI

  

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Diwani Msemo, akiongoza kikao na wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) kupitia Institute of Isotopes Co. Ltd. ya Hungary pamoja na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) cha kujadili taratibu za usafirishaji wa mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyotumika katika matibabu ya saratani.
Gábor Kaszás kutoka Institute of Isotopes Co. Ltd. ya nchini Hungary akichangia mada katika kikao cha majadiliano kuhusu taratibu za usafirishaji salama wa mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyotumika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCi kwa ajili ya matibabu ya saratani.
Wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) wakifuatilia kwa makini majadiliano wakati wa kikao cha kujadili  taratibu za usafirishaji salama wa mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyotumika katika matibabu ya saratani.



12/08/2026 Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), kwa kushirikiana na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), limekubaliana na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kuanza mchakato wa kusafirisha mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi yake katika mashine za matibabu ya mionzi kwa wagonjwa wa saratani.



Makubaliano hayo yamefikiwa leo jana katika kikao kilichowakutanisha Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dkt. Diwani Msemo, ujumbe wa IAEA kupitia kampuni ya Institute of Isotopes Co. Ltd kutoka nchini Hungary, ukiongozwa na Mr. Gábor Kaszás, pamoja na wajumbe kutoka TAEC.



Kwa mujibu wa makubaliano hayo, mabaki ya vyanzo hivyo vya mionzi yatasafirishwa kwenda nchini Hungary kwa ajili ya kuhifadhiwa na kufanyiwa mchakato wa kuyahuisha kwa matumizi mengine.


Vyanzo hivyo aina ya Cobalt vilitumika katika mashine za tiba ya mionzi kwa vipindi mbalimbali kuanzia mwaka 2008, huku vingine vikitumika katika vipindi vya mwaka 2014 hadi 2020 na mwaka 2025. Baada ya nguvu ya vyanzo hivyo kupungua na kutofikia kiwango kinachohitajika kwa ajili ya matibabu, ORCI ilinunua vyanzo vipya ili kuhakikisha huduma za matibabu ya saratani zinaendelea kutolewa kwa kuzingatia viwango vya ubora.



Mchakato wa kuondoa na kusafirisha mabaki ya vyanzo vya mionzi ni utaratibu wa kawaida unaotekelezwa kwa kushirikisha mamlaka husika za ndani, TAEC na IAEA kwa kuzingatia taratibu za usalama katika usimamizi wa vyanzo vya mionzi.



Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi yake yanadhibitiwa na kusimamiwa kwa usalama huku vyanzo vipya vikiendelea kutumika katika kutoa huduma za matibabu ya mionzi kwa wagonjwa wa saratani.
read more

WAZAZI WAHIMIZWA KUWACHANJA WATOTO KINGA YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

Watumishi wa Wizara ya Fedha wakimsikiza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Frank Rutachunzibwa wakati akitoa elimu ya magonjwa ya saratani kwenye zoezi la upimaji afya linalofanyika kwa wafanyakazi hao Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mali za Serikali kutoka Wizara ya Fedha, Choto Sendo akiuliza swali kuhusu magonjwa ya saratani wakati wa zoezi la upimaji afya linalofanywa na waatalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI)  kwa watumishi wa wizara hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kinga wa  Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Crispin Kahesa , akitoa elimu ya magonjwa ya Saratani kwa watumishi wa Wizara ya Fedha wakati wa zoezi la upimaji afya linalofanyika kwa watumishi hao Mtumba jijini Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Fedha wakimsikiza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Frank Rutachunzibwa wakati akitoa elimu ya magonjwa ya saratani kwenye zoezi la upimaji afya linalofanyika kwa wafanyakazi hao Mtumba jijini Dodoma.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Frank Rutachunzibwa, akieleza umuhimu wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka 9 hadi 14  wakati wa zoezi la upimaji afya linalofanyika kwa Watumishi wa Wizara ya Fedha iliyopo Mtumba jijini Dodoma


Na Mwandishi wetu – Dodoma

10/08/2026 Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwapeleka watoto wao wa kike wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa huo unaoongoza kwa vifo miongoni mwa saratani za uzazi kwa wanawake.


Rai hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Frank Rutachunzibwa, wakati akitoa mada ya uelimishaji kuhusu saratani kwa watumishi wa Wizara ya Fedha, Mtumba jijini Dodoma.


Dkt.Rutachunzibwa alisema chanjo hiyo hufanya kazi vizuri zaidi kwa watoto ambao bado hawajaanza kujamiiana kwani huwapa kinga dhidi ya maambukizi yanayoweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi baadaye katika maishani yao.

Alibainisha kuwa kila mwaka maelfu ya wanawake hupoteza maisha kutokana na saratani hiyo huku sababu kubwa ikiwa ni kuchelewa kugundua ugonjwa huo. 
“Kati ya wagonjwa wengi tunaowaona, idadi kubwa hufika hospitalini wakiwa katika hatua za mwisho” alisema.


Dkt. Frank Rutachunzibwa aliongeza kuwa pamoja na saratani ya mlango wa kizazi, zipo pia saratani nyingine zinazowaathiri watanzania wengi ikiwemo saratani ya matiti, tezi dume na mfumo wa chakula.

Daktati huyo Bingwa wa Magonjwa ya Saratani alisisitiza umuhimu wa kujichunguza  mapema na kufika hospitalini mara kwa mara kwa uchunguzi huku akionya kuwa watu wengi bado wanakimbilia tiba mbadala badala ya matibabu ya kisasa.


“Saratani inatibika kama magonjwa mengine. Ni muhimu kujipenda, kujichunguza na kutafuta matibabu sahihi bila kuchelewa lakini bado kuna imani potofu na mwitikio mdogo wa huduma za kinga, hali inayochangia wagonjwa wengi kugundulika katika hatua za mwisho za ugonjwa”, alisisitiza.


Alitaja baadhi ya vihatarishi vya saratani kuwa ni pamoja na mtindo usiofaa wa maisha, uvutaji wa sigara, pamoja na sababu za kinasaba. Pia alibainisha kuwa wanaume wanaweza kupata saratani ya matiti ingawa ni kwa kiwango kidogo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mali za Serikali, Choto Sendo aliishukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kwa kutoa elimu ya magonjwa ya saratani na yasiyo ya kuambukiza kwa watumishi wa Wizara hiyo na kusema kuwa elimu waliyoipata pamoja na upimaji watakaofanyiwa utawasaidia kujua hali za afya zao.


“Ninaishauri ORCI kuendelea kufanya tafiti ili kubaini sababu za ongezeko la saratani katika baadhi ya maeneo ya nchi, ikiwemo Kanda ya kaskazini ,Nyanda za juu kusini, Kanda ya Ziwa na Dar es Salaam, ni muhimu kuelewa chanzo cha tatizo ili kuweka mikakati madhubuti ya kinga badala ya kuendelea kutoa matibabu pekee”, alisema Sendo.


Saratani ya mlango wa kizazi ni miongoni mwa saratani zinazoongoza kwa vifo vya wanawake nchini, huku changamoto kubwa ikiwa ni uelewa mdogo na kuchelewa kwa uchunguzi na matibabu. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, chanjo kwa watoto wa umri wa miaka 9 hadi 14 ni njia muhimu ya kinga dhidi ya ugonjwa huo sambamba na uchunguzi wa mara kwa mara kwa watu wazima. 
read more

MAKAMU WA RAIS DKT NCHIMBI AMJULIA HALI RAIS MSTAAFU DKT.KIKWETE NYUMBANI KWAKE

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemtembelea na kumjulia hali, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika makazi yake, Kawe Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 10 Agosti 2026.




read more

RAIS MWINYI AFANYA UTEUZI



 

read more